most popular

Thursday, 20 October 2016

News Kenya

The Man who was Gang raped and finally speaks he wants to commit suicide

Kamili:Aliyelawitiwa na Watu Sita Akituhumiwa Kuwa na Mke wa Mtu Kingono Azungumza
“Ni kweli mimi ndiye niliyetendewa ukatili ule. Natamani kujiua kwani mambo yale nayasikia tu mungu anajua

“Nimefedheheka sana, sina mahala pa kuficha aibu hii kubwa. Kila nikikumbuka kuwa nina wake wawili na watoto, wazazi, marafiki na ndugu, bora hata wangeniua kuliko kuniacha nazidi kudhalilika hivi. Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu.

Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.

“Siku hiyo, saa tatu asubuhi mama Lilly alinipigia simu huku analia, akasema kwamba mumewe kampiga na kumfukuza nyumbani hivyo anaomba kuonana na mimi kwa ajili ya ushauri ila alitaka tukutane naye maeneo ya Mtongani, Mbagala au Tandika.

“Nilikataa, nikamwambia aje kwenye Ukumbi wa Maembe ninakotoaga mafunzo mbalimbali kwa vijana. Ukumbi huo upo karibu na nyumba hiyo ya kulala wageni kulikotokea tukio.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationery karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.

“Basi, nilipomwambia aje yeye maeneo haya, aliamua kunifuata. Alifika saa saba mchana huku akibubujikwa machozi, nilimsikiliza kwa makini matatizo yake mwishowe aliniomba nimkopeshe shilingi laki moja ili aende kwao, nilimjibu kwa pale sikuwa nazo labda mpaka Jumatatu.

News Kenya

About News Kenya -

Number news source for kenyan news

Subscribe to this Blog via Email :